Historia
Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Arusha ilianzishwa ikiwa kama kambi ya kutibu majeruhi katika vita kuu ya kwanza ya Dunia mwaka 1915 na ilizinduliwa rasmi kama hospitali ya mkoa tarehe 26.11.1926. Hatimaye ilipandishwa hadhi na kuwa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa mnamo tarehe 12.11.2010.
Hospitali hii ina uwezo wa kubeba vitanda 500 ila kwa hivi sasa ina vitanda 379. Hospitali ina Idara Kuu saba ambazo ni Idara ya Utawala, Dharura na ajali, Uzazi, Watoto, Upasuaji, Upasuaji (Mifupa) na Idara ya Tiba. Vilevile hospitali ina vitengo kumi na sita (16) ambavyo ni Famasi, Maabara, Mionzi, Meno, Macho, “Anaesthesia”, Masikio Pua na Koo (ENT), Magonjwa ya njia ya mkojo, Afya ya Akili, Mazoezi ya Viungo, Uhasibu, Manunuzi, BIMA ya afya, kitengo cha ubora wa huduma (QI) na HDU na Kitengo cha Ustawi wa Jamii.
Hospitali hii inahudumia wagonjwa wa nje kati ya 320 hadi 540 kwa siku, Wagonjwa wa marudio kati ya 250-350 kwa siku (Pamoja na CTC). Wagonjwa wapya watu wazima kati ya 60-120 kwa siku, Watoto 30-50 kwa siku. Wagonjwa wanaolazwa ni kati ya 70-120 kwa siku, Wanaojifungua kawaida 15-40 kwa siku, Wanaojifungua kwa upasuaji 5-15 kwa siku.
Hospitali ina watumishi wa Kada mbalimbali kama ifuatavyo; madaktari Bingwa 15 katika fani za upasuaji, magonjwa ya Ndani, Upasuaji mifupa, Pua koromeo na masikio, magonjwa ya njia ya mkojo, magonjwa ya wakinamama na uzazi, magonjwa ya dharura (EMD). Pamoja na hao hospitali inao madaktari 30 na madaktari wasaidizi AMO – 12. Hali kadhalika tunao wauguzi wa viwango mbalimbali kama ifuatavyo:- Specialist Nurse wawili (2) katika michepuo ya “Critical care” na Ukunga (Midwifery), Afisa wauguzi 22, Maafisa wauguzi msaidizi 128 na wauguzi 82. Na watumishi wa Kada nyingine 194 inayopelekea jumla ya watumishi 484