ICT

Kitengo cha TEHAMA ni mojawapo ya vitengo vilivyopo ndani ya Hospitali. Kitengo  hiki kimekuwa kikitekeleza majukumu yake ya kila siku kwa kuzingatia Sera, Sheria, Kanuni na Miongozo mbalimbali. Jukumu kubwa la wataalam wa sekta hii ni kwamba wanahusika katika kuratibu, kufuatilia na kutathmini shughuli mbalimbali za kitengo.

Kitengo hiki kinasimamia mifumo ya kiserikali na shughuli za TEHAMA katika Hospitali ya mkoa ya Mount Meru

Ofisi ya Mganga mfawidhi kupitia kitengo cha TEHAMA imekuwa ikisimamia usimikwaji wa mifumo mbali mbali kama GoT HoMIS, HCMIS-LAWSON, GePG, LabNet Pamoja na kuhakikisha mifumo hii inasaidia kuboresha shughuli za Serikali.


KAZI ZA KITENGO CHA TEHAMA

  1. Kusimamia na kuhakikisha shughuli zote zinazofanyika kwa njia ya kielekroniki ziko katika hali nzuri.

  2. Kutoa huduma katika kila seksheni/kitengo juu ya mtandao ,changamoto za kompyuta ,printers,scanners n.k

  3. Kuhakikisha huduma zote za kielekroniki zinapatikana bila kukwama.

  4. Kusimamia mifumo iliyosimikwa katika Hospitali ya mkoa ya Mount Meru.

  5. Kutoa huduma katika kazi zingine zote zinazohusiana na kitengo.