Huduma za Famasia
IDARA YA PHARMACY
Idara ya Pharmacy katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa,Mount Meru inatoa huduma bora za dawa na zenye viwango kwa wagonjwa wa nje na waliolazwa wanaofika kuhudumiwa.Idara ya Pharmacy ina wajibu wa kuhakikisha upatikanaji wa dawa muhimu kwa muda wote; dawa zenye ubora,zinazohifadhiwa kwa viwango vinavyohitajika na zinazotumika kwa mgonjwa Kama inavyostahili kwa kizingatia kanuni sita za matumizi sahihi ya dawa,ambazo ni ;-
-
Mgonjwa sahihi
-
Dawa sahihi
-
Dozi sahihi
-
Muda sahihi
-
Njia sahihi ya kutolea dawa
-
Bei sahihi kwa mgonjwa.
MUUNDO WA IDARA YA PHARMACY
Idara ya pharmacy katika Hospitali ya rufaa ya mkoa-Mount meru ina vitengo vinne,lengo la kuwa na vitengo hivi ni kuboresha utoaji wa huduma za dawa,Vitengo hivyo ni ;-
-
Pharmacy ya BIMA
-
Pharmacy ya Wagonjwa wa nje
-
Pharmacy ya kutoa dawa kwa wanaoishi na virusi vya UKIMWi ( WAVIU)
-
Bohari ya dawa na ofisi
-
Duka la dawa la hospitali
PHARMACY YA BIMA.
Pharmacy ya Bima inatoa huduma kwa wateja/wagonjwa wanaohudumiwa na mashirika mbali mbali ya BIMA za afya,mfano ,mfuko wa bima ya afya-taifa (NHIF).Pharmacy hii ipo katika jengo maalumu kwa ajili ya wagonjwa wa BIMA tu.
PHARMACY YA WAGONJWA WA NJE.
Pharmacy ya wagonjwa wa nje inatoa huduma kwa wateja/wagonjwa wasio kuwa na BIMA yeyote ya afya,aidha pia watoto,wazee na makundi yote ya misamaha yanahudumiwa na pharmacy hii,pharmacy hii hutoa huduma kwa wagonjwa wote ambao hawajalazwa. Pharmacy hii inatoa huduma zake masaa 24 ili kuwahudumia wagonjwa ki ufanisi.
PHARMACY YA KUTOA DAWA KWA WANAOISHI NA VIRUSI VYA UKIMWI ( WAVIU)
Wanaoishi na virusi vya UKIMWI (WAVIU) wanapata huduma zote za dawa katika pharmacy hii maalumu kwa ajili yao,Pharmacy hii ipo ndani ya jengo mahususi kwa ajili ya WAVIU,hivyo mgonjwa hata sumbuka kwenda sehemu nyingine,atahudumiwa hapohapo.
BOHARI YA DAWA NA OFISI
Kuna bohari ya kuhifadhia dawa ili kuzitunza kiufanisi,hapa dawa zote zinatunzwa kwa kuzingatia viwango stahiki. Chanzo kikuu cha kununulia dawa zetu ni Bohari ya dawa ya Taifa ( MSD) na endapo zitakosekana MSD,dawa hizo hununuliwa kwa Mshitiri wa Mkoa kwa kufuata taratibu na sheria.Dawa zote husambazwa kwenda wodini au katika vitengo vingine kwa mfumo wa ki-electronic uitwao GoT HoMIS. Sambamba na bohari ya dawa kuna ofisi ambapo kumbukumbu zote za idara zinatunzwa.
DUKA LA DAWA LA HOSPITALI.
Ili kuboresha huduma na kupunguza adha kwa wagonjwa,hospitali imeanziasha duka la kisasa la dawa ili dawa zitakazo kosekana katika pharmacy ya hospitali zinunuliwe katika duka la hospitali,hii itapunguza adha kwa mgonjwa na kuongeza mapato kwa hospitali.