Uratibu wa Afya na Mipango
Uratibu Wa Afya Na Mipango
Idara ya Uratibu wa afya na Maipango inaratibu na kusimamia kazi zifuatazo
-
Kutoa maelekezo na ushauri wa kiutawala na usimamizi wa rasilimali za hospitali.
-
Kuandaa mipango ya hospitali ya kushirikaiana na wakuu wa idara na utekelezaji wa mipango hii kupitia bajeti ya iliyoandaliwa kwa kila mwaka.
-
Kutoa tafsiri sahihi ya miongozo, sera na mikakati iliyoandaliwa na wizara ya afya ,maendeleo ya jamii ,jinsia na watoto kwa ajili ya utekelezaji ndani ya hospitali.
-
Kuandaa mipango kabambe ya hospitali kila mwaka.
-
Kuandaa taarifa za utekelezaji za kila wiki, mwezi, robo mwaka na mwaka mzima za mpango wa kupelekwa kwenye mamlaka husika.
-
Kwa kushirikiana na wakuu wa idara, kuandaa taarifa na fedha, majengo, muhtasari ya vikao mbalimabli zitakazowasilishwa kwenye vikao vya menejimenti kwa ajili ya maamuzi.
-
Kwa kushirikiana na timu ya usimamizi wa hospitali, kuratibu na kusimamia shughuli za uboreshaji huduma kwa wateja.