Uhasibu na Fedha
KITENGO CHA UHASIBU
Majukumu ya kitengo cha Fedha na Uhasibu yamegawanyika kwenye nyanja zifuatazo:
Kuwezesha Malipo:
- Kuandaa na kuingiza malipo kwenye mtandao wa malipo
- Kuchukua hundi zamalipo kutoka Hazina ndogo
- Kupeleka fedha tasilimu na hundi benki
- Kutayarisha taarifa za mwezi za malipo
- Kuwalipa watumishi fedha taslimu au hundi na kuwalipa watoa huduma kwa hundi
- Kutunza daftari la hesabu
Hesabu za Mwisho wa Mwaka:
- Kutayarisha Makadirio ya bajeti na kudhibiti matumizi
- Kuandaa taarifa ya matumizi ya robo mwaka, nusu mwaka na mwaka mzima kwa ajili ya kuiwasilisha kwa Mhasibu Mkuu wa Serikali
- Kujibu hoja zote na maoni ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG)
- Kuandaa taarifa ya hesabu za mwisho wa mwaka na kuziwasilisha kwa Mhasibu Mkuu wa Serikali na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali
Ukusanyaji Mapato:
- Kukusanya Mapato
- Kusimamia mapato kwa mujibu wa sheria na miongozo
Ukaguzi wa Awali:
- Kuhakiki nyaraka za malipo kama zimezingatia taratibu za malipo ikiwa ni pamoja na kuidhinishwa
- Kuhakikisha kama sheria, kanuni na miongozo na nyaraka za fedha kama zimezingatiwa
- Kuhakikisha malipo yatakayofanyika hayavuki bajeti ya kasma husika