Sheria

Kitengo cha Sheria ni mojawapo ya vitengo vilivyopo Hospitali. Kitengo hiki kimeundwa ili kuisaidia Hospitali katika masuala mbalimbali ya kisheria.


1.1. MAJUKUMU YA KITENGO CHA SHERIA

  1. Kutoa ushauri wa kisheria na kuisaidia Hospitali katika kutafsiri sheria, mikataba, makubaliano na nyaraka mbalimbali za kisheria kwa kushirikiana na Mkurugenzi wa Huduma za Sheria wa Wizara ya Afya na Mwanasheria Mkuu wa Serikali

  2. Kufanya kazi mbalimbali katika Bodi za Kudumu na Kamati mbalimbali za uchunguzi za muda;

  3. Kushiriki katika Majadiliano na Mikutano mbalimbali ambayo inahitaji utaalamu wa Kisheria.

  4. Kusaidia katika kutoa tafsiri za Sheria mbalimbali katika  Hospitali

  5. Kuandaa na kupitia nyaraka mbalimbali za Kisheria kama vile Mikataba, makubaliano, Amri, Taarifa, Vyeti na nyaraka za kuhamisha umiliki;

  6. Kufanya kazi nyingine kama zitakavyoelekezwa na Mganga mfawidhi wa Hospitali.