News

HOSPITALI YA MT. MERU YAENDELEA KUSHIKA CHATI KWA USAFI NA UTUNZAJI WA MAZINGIRA

Posted on: 2025-04-26 14:01:00

Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Arusha Mount Meru, imepata tuzo ya mshindi wa pili kwa utunzaji wa mazingira na upandaji miti katika tuzo zilizoandaliwa na ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Paul Makonda na kukabidhiwa na Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa nishati Mhe. Doto Biteko katika maadhimisho ya miaka 61 ya Muungano wa Tanganyila na Zanzibar yaliyofanyika Jijini Arusha.

Akizungumza mara baada ya kupokea tuzo Kaimu Mganga Mfawidhi Hospitali ya Mount Meru, Dkt. Kipapi Mlambo ameishukuru Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Arusha kwa tuzo hiyo na kuahidi kuwa wataendelea kutunza mazingira ili kuwa hospitali ya mfano kila wakati.

“Kwa niaba ya Menejimenti ya Hospitali ya Mkoa wa Arusha ninapenda kutoa shukrani zangu za dhati kwa ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Arusha kwa zawadi hii na tunaahidi kuendelea kutunza mazingira ili hospitali pia iendelee kuwa ya mfano zaidi”.Amesema Dkt. Kipapi.

Sambamba na hayo Dkt. Kipapi amewataka wananchi wote wenye changamoto za Kiafya kufika katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Arusha Mount Meru ili kupata matibabu kwani tuzo za mazingira zinaenda sambamba na utoaji bora wa huduma za afya.

Tuzo hii ya utunzaji wa mazingira kwa Hospitali ya Mount Meru ni ya pili mfululizo ndani ya kipindi cha mwezi mmoja ambapo mwanzoni mwa mwezi wa nne walipokea tuzo ya mshindi namba moja ya utunzaji wa mazingira kitaifa kutoka Wizara ya afya kati ya Hospital zote za Rufaa Nchini.

Latest news

Mwanga Wa Afya
Mwanga Wa Afya

2025-04-17 08:44:40

PRESS RELEASE ON MPOX THREAT
PRESS RELEASE ON MPOX THREAT

2024-08-19 13:44:21

THE IMPORTANCE OF THE GENDER DESK
THE IMPORTANCE OF THE GENDER DESK

2024-06-26 10:00:00

Quick feedback
Book an appointment