News

UFAFANUZI KUHUSU TAARIFA ILIYOSAMBAA KATIKA MITANDAO YA KIJAMII KUHUSU HOSPITALI KUZUIA NDUGU KUCHUKUA MWILI.

Posted on: 2025-08-12 09:01:11

Mnamo 09/08/2025 majira ya saa nne na robo usiku, Hospitali ilipokea mgonjwa wa ajali alivejulikana kwa jina la Mohamed Ally umri wa miaka 20. Mgoniwa alipokelewa na kuanza kupatiwa matibabu na ndugu zake walifika majira ya saa nane usiku baada ya kupigiwa simu ya kupewa taarifa na Hospitali.

Mgonjwa alifanyiwa uchunguzi ikiwemo kupigwa X Ray, CT Scan a Vipimo mbalimbali vya maabara. Vile vile kutokana na hall aliyokuwa nayo, alianzishiwa matibabu ya dharura na kuwekwa chini ya uangalizi maalum wa madaktari. Gharama za huduma zote zilizotolewa ziligharimu kiasi cha Shilingi. 910,000.

Ndugu wa mgonfwa walifika saa nane usiku na hali ya mgonjwa ilizidi kubadilika na kuwa mbaya pamoja na juhudi zote za kitabibu zilizokuwa zinafanywa ndani ya kitengo cha huduma za dharura ambapo dugu walipewa taarifa. Majira ya saa nane usiku mgonjwa alifariki dunia.

Mnamo tarehe 11/08/2025 saa mbili asubuhi ndugu wa marehemu walifika kuchukua mwili wakiongozana na marafiki wa marehemu ambao walikuwa ni vijana wa bodaboda.

Ndugu walipewa bili a gharama za matibabu na kuelekezwa utaratibu wa kulipia wakati mwill ukiandaliwa ambapo walilipa na kukabidhiwa mili pasipo changamoto yoyote mnamo saa nne asubuhi. Aidha wakati wa kuchukua mwili vijana wa bodaboda walifanya vurugu eneo la motuari wakidai bili waliyopewa ni kubwa na isiyoeleweka.

Hospitali inatekeleza maelekezo ya Serikali ya kutokuzuia Milli ya marehemu kwa sababu ya kutokulipwa kwa bili a hivyo INAKANUSHA taarifa za upotoshaji na zene kuleta taharuki kwamba mwill wa marehemu ulizuiliwa kuchukuliwa kutokana na bili kutokulipwa.

Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Arusha Mount Meru inawahakikishia wananchi kuwa itaendelea kutoa huduma kwa kuzingatia miongozo iliyotolewa a Wizara ya Afya na itaendelea kuhakikisha kila mgonjwa anapata haki ya kupatiwa huduma kwanza pasipo kikwazo chochote ikiwemo cha kukosa fedha

Imetolewa na Ofisi ya Manga Mfawidhi

Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Arusha, Mt. Meru

Latest news

Mwanga Wa Afya
Mwanga Wa Afya

2025-04-17 08:44:40

PRESS RELEASE ON MPOX THREAT
PRESS RELEASE ON MPOX THREAT

2024-08-19 13:44:21

THE IMPORTANCE OF THE GENDER DESK
THE IMPORTANCE OF THE GENDER DESK

2024-06-26 10:00:00

Quick feedback
Book an appointment